Imeshindwa kupakua, kufungua au kutuma faili za maudhui

Android
iOS
Ikiwa huwezi kupakua, kufungua au kutuma faili za maudhui, sababu ya kawaida ya hili ni muunganisho dhaifu wa intaneti. Tunapendekeza:
  • Uwashe simu yako upya au uizime kisha uiwashe tena.
  • Usasishe WhatsApp iwe toleo la hivi karibuni.
  • Ujaribu kuunganisha kwenye data ya vifaa vya mkononi ikiwa unatumia Wi-Fi au Wi-Fi ikiwa unatumia data ya vifaa vya mkononi.
  • Uwasiliane na kampuni inayokupa huduma za simu.
Tatizo linaweza pia kuhusishwa na kadi yako ya SD. Angalia ikiwa kadi yako ya SD ina:
  • Nafasi ya kutosha ya kuhifadhi. Huenda ukahitaji kufuta data ya WhatsApp kwenye kadi yako ya SD ili upate nafasi ya kupakua maudhui.
  • Umezima hali ya kusoma tu.
Ikiwa bado unatatizika, huenda kadi yako ya SD imeharibika na unahitaji kubadilisha mipangilio ya kadi au ununue kadi mpya ya SD.
Kumbuka: Ikiwa huwezi kufungua faili ya PDF iliyopakuliwa kwenye simu yako, hakikisha kuwa umesakinisha programu ya kisomaji cha PDF kwenye simu yako. Ikiwa faili inalindwa kwa nenosiri, thibitisha kuwa una ruhusa ya kuiangalia. Ikiwa bado faili haifunguki, jaribu kuzima na kuiwasha tena simu yako.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La