Vidokezo vya usalama kwenye akaunti

Ili uweke akaunti yako ya WhatsApp salama, fuata vidokezo hivi:
  • Usishiriki msimbo wako wa usajili au PIN ya uthibitishaji wa hatua mbili kati yako na wengine.
  • Washa kipengele cha uthibitishaji wa hatua mbili kisha uweke anwani ya barua pepe ikiwa utasahau PIN yako.
  • Weka nenosiri la ujumbe wa sauti kwenye simu yako ambalo ni vigumu kulikisia ili kuzuia mtu yeyote kufikia ujumbe wako wa sauti.
  • Angalia vifaa vyako vilivyounganishwa mara kwa mara. Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp > Vifaa Vilivyounganishwa ili ukague vifaa vyote vilivyounganishwa kwenye akaunti yako. Ili uondoe kifaa kilichounganishwa, gusa kifaa > Ondoka.
  • Weka msimbo kwenye kifaa ili ufahamu ni nani ambaye amefikia simu yako. Mtu aliye na uwezo wa kufikia simu yako anaweza kutumia akaunti yako ya WhatsApp bila ruhusa yako.
Tunapendekeza ushiriki ushauri huu na jamaa na marafiki ili uwasaidie kulinda akaunti zao za WhatsApp.
Kumbuka: Ukipokea barua pepe ambazo hujaombwa ili kuweka upya PIN yako ya uthibitishaji wa hatua mbili au msimbo wa usajili, usibofye viungo vyovyote. Mtu fulani anaweza kuwa anajaribu kuhakiki namba yako ya simu kwenye WhatsApp.

Rasilimali

Je, hili linajibu swali lako?

Ndiyo
La