Jinsi ya kuchanganua msimbo wa QR wa WhatsApp

Android
iPhone
Unaweza kuchanganua msimbo wa QR wa WhatsApp ili kuongeza maelezo ya mawasiliano ya rafiki au mwanafamilia kwenye WhatsApp.
Kuchanganua msimbo wa QR wa WhatsApp
Kuchanganua wewe binafsi
 1. Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio.
 2. Gusa aikoni ya QR inayoonyeshwa karibu na jina lako.
 3. Gusa CHANGANUA MSIMBO.
 4. Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR ili kuuchanganua.
 5. Gusa ONGEZA.
Kuchanganua kwa kutumia kamera yako kwenye WhatsApp
 1. Fungua WhatsApp > gusa Kamera
  .
 2. Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR ili kuuchanganua.
 3. Gusa ONGEZA.
Kuchanganua kutoka kwenye Matunzio
 1. Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio.
 2. Gusa aikoni ya QR inayoonyeshwa karibu na jina lako.
 3. Gusa CHANGANUA MSIMBO.
 4. Gusa aikoni ya Matunzio chini ya skrini.
 5. Chagua msimbo wa QR wa WhatsApp kutoka kwenye Matunzio au gusa Zaidi
  > Picha ili uchague kutoka kwenye Picha zako.
 6. Gusa SAWA.
 7. Gusa ONGEZA.
Kuchanganua kutoka kwenye skrini ya Anwani Mpya
 1. Fungua WhatsApp > gusa Soga mpya
  .
 2. Gusa aikoni ya QR karibu na Anwani mpya.
 3. Gusa CHANGANUA MSIMBO.
 4. Gusa ONGEZA.
Kuchanganua kutoka kwenye kamera ya WhatsApp
 1. Fungua WhatsApp > gusa Kamera
  .
 2. Chagua picha yenye msimbo wa QR ili kuuchanganua.
 3. Gusa ONGEZA.
Kuchanganua ndani ya soga
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Gusa aikoni ya kamera.
 3. Chagua picha yenye msimbo wa QR ili kuuchanganua.
 4. Gusa ONGEZA.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La