Kuhusu kutumia akaunti moja ya WhatsApp kwenye simu kadhaa au katika namba kadhaa za simu

Akaunti yako ya WhatsApp inaweza tu kuthibitishwa kwa kutumia namba moja ya simu uliyoisajili. Ikiwa una simu inayokubali kadi mbili ya SIM, tafadhali kumbuka kwamba bado ni lazima uchague namba moja ya kuthibitishia WhatsApp. Hakuna chaguo la kuwa na akaunti moja ya WhatsApp iliyothibitishwa na namba mbili tofauti za simu.
Unaweza kubadili akaunti yako ya WhatsApp hadi kwenye simu mpya bila kupokea msimbo kupitia SMS.
Ikiwa namba yako ya simu inatimiza masharti, unaweza kuithibitisha ukitumia kifaa chako cha zamani. WhatsApp itatuma arifa ya programu kwenye kifaa cha zamani ambacho kitatoa msimbo wenye tarakimu 6 ili uuweke kwenye kifaa chako kipya.
Ikiwa hutachagua chaguo hili, utaombwa uthibitishe namba yako ya simu kupitia SMS.
Ikiwa utajaribu kubadilisha akaunti yako ya WhatsApp mara kwa mara kati ya vifaa tofauti, kwa wakati fulani, unaweza kuzuiliwa kuthibitisha tena akaunti yako. Tafadhali usibadilishe mara kwa mara kati ya vifaa na namba tofauti.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La