Kuhusu kutumia akaunti moja ya WhatsApp kwenye simu kadhaa au katika nambari kadhaa za simu

Akaunti yako ya WhatsApp inaweza tu kuthibitishwa na nambari moja kwenye simu moja. Ukiwa una simu inayokubali SIM mbili, tafadhali kumbuka kwamba bado ni lazima uchague nambari moja ya kuthibitishia WhatsApp. Hakuna chaguo la kuwa na akaunti moja ya WhatsApp yenye nambari mbili za simu.
Ukijaribu kubadilisha akaunti yako ya WhatsApp mara kwa mara kati ya vifaa tofauti, kwa wakati fulani, unaweza kuzuiliwa kuthibitisha tena akaunti yako. Tafadhali usirudierudie kubadilisha kati ya vifaa na nambari tofauti.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La