Jinsi ya kuunda kiungo kifupi

Programu ya WhatsApp Business inakuwezesha kushiriki kiungo na wateja ili waweze kuanzisha soga na wewe moja kwa moja.
Mteja akifungua kiungo kifupi kwenye kifaa kilichosakinishwa WhatsApp, soga salama kati yenu wawili itafunguliwa kiotomatiki. Akifungua kiungo kifupi kwenye kivinjari cha tovuti, ataelekezwa kwenye ukurasa wa tovuti wenye taarifa za biashara yako na ujumbe wako chaguomsingi ukiwa umewekwa. Kuanzia hapo, anaweza kubofya ENDELEA NA SOGA ili aanze kupiga soga na wewe.
Kumbuka: Ikiwa umechagua kushiriki picha yako ya jalada na Kila mtu katika mipangilio yako ya faragha, picha yako ya jalada pia itaonekana kwenye ukurasa wa wavuti. Pata maelezo ya jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha kwenye makala haya.
Kuunda kiungo kifupi
Kiungo kifupi cha biashara yako huundwa kiotomatiki unapounda akaunti kwenye programu ya WhatsApp Business. Kufikia kiungo hiki kifupi:
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Chaguo zaidi
  > Zana za biashara.
 2. Gusa Kiungo kifupi ili uone kiungo kilichoundwa kiotomatiki.
Mara unapokifikia kiungo kifupi, unaweza:
 • Kugusa
  ikiwa unataka kunakili kiungo kifupi na kubandika kwingine kwenye tovuti yako au kwenye kurasa nyingine za Facebook.
 • Kugusa
  kama unataka kutuma kiungo moja kwa moja kwa wateja wako. Mtu yeyote aliye na kiungo anaweza kukutumia ujumbe.
 • Kugusa kitelezi ili kuweka kiolezo cha ujumbe kwa wateja kutumia wanapofungua kiungo kifupi.
 • Kugusa
  ili uunde na kuhariri ujumbe wako chaguomsingi.
Dokezo la kibiashara: Ujumbe chaguomsingi uliowekwa awali huwarahisishia wateja kuwasiliana na biashara yako wakiwa na maswali au hoja nyingine za kawaida.
Rasilimali zinazohusiana
Kuhusu kiungo kifupi kwenye iPhone
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La