Kuhusu kupiga simu kwenye kompyuta

Unaweza kupiga simu za sauti na za video bure kwa watu walio katika anwani zako ukitumia WhatsApp Desktop ikiwa umesakinisha programu hiyo kwenye kompyuta yako.
Unaweza kupiga simu kupitia kompyuta ya mezani kwenye:
  • Windows 10 64-bit toleo la 1903 au jipya
  • macOS 10.13 au matoleo mapya
Ili kupiga au kupokea simu kwenye WhatsApp Desktop, utahitaji:
  • Kifaa cha kutoa sauti na maikrofoni kwa simu za sauti na video.
  • Kamera kwa ajili ya simu za video.
  • Kuruhusu WhatsApp ifikie maikrofoni na kamera ya kompyuta yako. WhatsApp inahitaji kufikia maikrofoni ya kompyuta yako kwa ajili ya kupiga simu na kamera kwa ajili ya simu za video.
Kumbuka: Simu za kikundi haziwezi kutumika kwenye WhatsApp Desktop kwa wakati huu.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La